29 Septemba 2015 - 20:27
Magaidi 650 waangamia nchini Syria

Majeshi ya Syria na nguvu za wananchi wamefanya mashambulizi makali katika ngome za magaidi hao nchini humo katika kipindi cha hivi karibuni katika mji wa Alfua na Kufriya, mashambulio ambayo yamepelekea kuangamia magaidi 650 nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: habari hiyo imetangazwa leo na televishen ya Almayadin kuwa magaidi hao waliangamia kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano mji wa Alfua na Kufriya.
Mwandishi wa habari wa televishen hiyo baada ya kutangaza habari hii alisema: jeshi la Syria liliamua kufanya mashambulio makali katika ngome za vikundi hivyo vya kigaidi miezi iliopita na kuwaangamiza magaidi zaidi ya 650 nchini humo.
Aidha amebainisha kuwa jeshi la Syria na jeshi la nguvu za wananchi yalikubali kufanya makubaliano ya kusitisha vita kwa muda baada ya kuwaangamiza makamanda wa majeshi ya magaidi hao.
Vyombo vya habari vya Syria vyaeleza kuwa Hapo kambla kikundi cha (Ihrarusshamu) kilikuwa kinapinga suala la kusitisha vita kwa muda, ama baada ya kipigo hicho kikali kikundi hicho pia kililazimika kukubali suala hilo lakusitisha vita kwa muda.
Vikundi vya kigaidi viliopo dhidi ya serikali ya Syria muda mrefu vilikuwa katika juhudi kubwa yakutaka kuiteka miji hiyo inayokaliwa na mashia ya (Alfua, Kufria na Alzabadan) ama kutokana na juhudi za jeshi la Syria na nguvu za wananchi magaidi hao wameshindwa kufikia malengo yao katika miji hiyo.
mwisho wa habari/290